Jumapili 27 Aprili 2025 - 06:48
Je, kuchagua jinsia ya mtoto ni jambo lililo ndani ya uwezo wa mwanadamu?

Aya ya 49 ya Suratu Shura inaeleza kwamba; Mwenyezi Mungu ndiye mmiliki wa ulimwengu na kuwa kila neema na rehema hutoka kwake. Yeye humruzuku amtakaye mtoto wa kike au wa kiume, na huwafanya baadhi ya watu kuwa tasa. Aya hii inaonesha kuwa kuamuliwa kwa jinsia ya mtoto na uwezo wa kupata watoto ni ishara ya uwezo na umiliki wa Mwenyezi Mungu, na mwanadamu ana mipaka katika jambo hili.

Kwa mujibu wa taarifa ya  Shirika la Habari la Hawza, uwezo wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji na uendeshaji wa ulimwengu hauna mipaka, na kuamuliwa kwa jinsia ya watoto kunategemeana na mapenzi yake. Hili linaonesha wazi udhaifu wa mwanadamu mbele ya nguvu ya Mwenyezi Mungu Aliye na uwezo wa hali ya juu.

Katika maswali na majibu yajayo, tutaangazia hoja hii kwamba kuchaguliwa kwa jinsia ya watoto kunategemea matakwa ya Mwenyezi Mungu, wala si mwanadamu.

Swali:
Je, kuchagua aina ya mtoto kunapatikana kwa uwezo wa mwanadamu?

Jawabu la muhtasari:
Aya za Qur'ani zinaeleza wazi kuwa; kuwa na mtoto wa kike au wa kiume kunapatikana tu kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, licha ya juhudi zote, pamoja na maendeleo ya kielimu tuliyo nayo, lakini juhudi hizo zimeshindwa kuwa na uwezo wa kuchagua katika jambo hili, na udhaifu wa mwanadamu katika masuala haya ni dalili ya uamiliki, uweza na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

Jawabu kwa upana:
Jawabu la swali hili linaweza kupatikana kwa kurejea Aya ya 49 ya Suratu "Shura". Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kubainisha ukweli huu kuwa kila aina ya neema na rehema katika ulimwengu huu hutoka kwake, na kuwa hakuna yeyote anayemiliki chochote kutoka kwake, amelitaja jambo la jumla pamoja na mfano wake wa wazi, kwa kusema:  "Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; Yeye huumba apendavyo"


“للَّهِ مُلكُ ٱلسَّمَـٰوَ ٰ⁠تِ وَٱلأَرۡضِۚ یَخلقُ مَا یَشَاءُۚ یَهَبُ لِمَن یَشاءُ’”

Mfano wa wazi wa ukweli huu kuwa hakuna mtu anayemiliki chochote, na kwamba kila kitu hutoka kwa Mwenyezi Mungu ni huu:  
"Humruzuku amtakaye mtoto wa kike, na humruzuku amtakaye mtoto wa kiume"


{یَهَبُ لِمَن یَشَاۤءُ إِنَـٰثا وَیَهَبُ لِمَن یَشَاءُ ٱلذُّكُورَ}
 

(au kama akitaka, huwapa wote wawili: wa kiume na wa kike; na humfanya kuwa tasa amtakaye)  

{ أَوۡ یُزَوِّجُهم ذُكرَانا وَإِنَـٰثا وَیَجعَلُ مَن یَشَاءُ عَقِیمًا إِنَّهُۥ عَلِیم قَدِیرࣱ }(1)

Cha kushangaza ni kwamba hakuna mtu, si katika zama za kale au leo hii ambapo sayansi imepiga hatua kubwa, aliyekuwa na uwezo wa kuchagua katika suala hili, licha ya juhudi zote, bado hakuna aliyeweza kumpa mtoto mtu aliyekuwa tasa kwa kweli, wala kubainisha jinsia ya mtoto kwa mujibu wa matakwa ya mwanadamu. Ingawa haiwezi kupingwa kuwa baadhi ya vyakula na dawa zinaweza kuongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume au wa kike, lakini lazima tujue kuwa haya yanaongeza tu uwezekano, lakini hayatoi matokeo ya uhakika.  
Na huu ni mfano wa wazi wa udhaifu wa mwanadamu kwa upande mmoja, na dalili dhahiri ya uamiliki, uweza, na uumbaji wa Mwenyezi Mungu kwa upande mwingine. (2)

Rejea:

(1) Suratu Shura, Aya ya 50.  
(2) Imenukuliwa kutoka katika kitabu cha "Tafsiri Amthal", kilichoandikwa na Ayatullah al-Udhma Makarim Shirazi, Dar al-Kutub al-Islamiyya, chapisho la ishirini na sita, Juzuu ya 20, uk. 508

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha